5 Mei 2025 - 23:29
Source: Parstoday
Familia za mateka Wazayuni: Njia pekee ya kuwarejesha mateka ni kuipindua serikali ya Netanyahu

Familia za mateka Wazayuni wanaoshikiliwa Ghaza zimesema, anachopigania waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu ni kurefusha vita kwa malengo yake ya kisiasa, kwa hiyo njia pekee ya kuwarejesha mateka wao ni kuipindua serikali ya Netanyahu, na kwamba lengo hilo litafikiwa kwa wazayuni wote kumiminika mabarabarani.

Familia hizo za mateka Wazayuni wanaoshikiliwa na wanamuqawama wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimekosoa utendaji wa Netanyahu na kusisitiza kuwa, kuitisha vikosi zaidi vya askari wa akiba kwa ajili ya vita vya Ghaza kutasababisha vifo zaidi tu vya watoto wao.

Familia za wafungwa hao wa Kizayuni zimeendelea kueleza kwamba, njia pekee ya kuwarejesha mateka wa Kizayuni walioko Ghaza ni kuipindua serikali ya Netanyahu na kuleta mabadiliko; na kupinduliwa serikali hiyo ndilo takwa la awamu ya sasa, kwa hiyo inapasa watu wote waingie barabarani kwa ajili ya kulipindua baraza hilo la mawaziri la Netanyahu.

Jamaa wa wazayuni hao wamesema, badala ya kuwaokoa mateka, Netanyahu anatuma wanajeshi zaidi ili wakauawe huko Ghaza. Tunatoa wito kwa Mkuu wa Majeshi asitekeleze operesheni yoyote huko Ghaza kwa sababu itapelekea kuuawa mateka.

Familia hizo zimesisitiza kwa kusema: "ikiwa tunataka kuunda serikali na kulifunga faili la Oktoba 7, inapasa tufanye juhudi za kulipindua baraza la mawaziri la Netanyahu. Lazima tukomeshe mara moja vita huko Ghaza. Sisi tunamwambia Trump asiwaache mkono mateka na awe makini na mchezo wa Netanyahu".

Jamaa wa mateka Wazayuni vilevile wamesema, Netanyahu angali anaendelea kuwatoa mhanga askari wa Israel ili kuiokoa serikali yake.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha